Thursday, 22 March 2018

W WAPO Social Media

Ukikwama njia panda, kikwazo sio njia panda

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Tumezoea kufikiri ya kwamba, mtu akiwa anasafiri kwa kutumia njia ya miguu au baiskeli na hata gari kama akifika sehemu ya makutano maarufu kama njia panda; kisha akakosa kuona kibao kinachotambulisha kila njia inaelekea wapi; basi lawama zote hutupiwa hayo makutano/njia panda kwa kuwa kikwazo cha kukwamisha safari za wapitao sehemu hiyo!

Haya ni mazoea na kwa sehemu yana mantiki. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba “kukwama njia panda” kikwazo “sio hiyo njia panda”! Kikwazo ni kutokuifahamu tangu mwanzo njia sahihi ya kule unakoelekea! Kumbuka ya kwamba kuna watu wengi wanaotokea huko watokako na kufika hapo njia panda lakini hawakwamii hapo pamoja na kwamba bado hakuna kibao kinachoelekeza njia ziendako!

Hawa wasiokwama njia panda ni kwa sababu tangu huko walikotoka wanajua njia sahihi ya kule waendako na ndio maana wakifika hapo hawakwami kabisa. Ama walikwisha kupitia hapo huko nyuma na kwa hiyo sio mara ya kwanza kufika sehemu hiyo!

Au hata kama ni wageni kabisa bado inaonesha ya kuwa kabla ya kuanza safari wahusika walipata maelekezo kamili kuhusu njia sahihi ya kule waendako. Si ajabu walikuwa wanatarajia kufika sehemu hiyo ya njia panda isiyo na kibao chenye mwongozo. Kwa hicho kilikuwa ni kiashiria cha kutambua ni upande gani wa njia sahihi ya kuwafikisha wanakokwenda.

“Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.” (Isa.35:8)

Ni matumaini yangu kwamba umesherehekea Pasaka kwa amani na umesalimika na changamoto zinazoendelea katika jamii. Ni wakati sasa wa kujitathmini kama tumekwama njia panda tatizo sio hiyo njia panda, tatizo ni kutokujua njia sahihi ya tuendako tangu mwanzo.

Ufumbuzi sio kuilalamikia njia panda, wala sio kulalamikia walioshindwa kuweka kibao elekezi, ufumbuzi ni kutafakari upya ni wapi hasa tunakwenda, na kama tunakujua tunakokwenda kabla ya kuanza safari yenyewe.

Utasema nimetumia mafumbo sana. Mafumbo nayo husaidia katika kubungua bongo na ni mojawapo ya njia bora za kujifunza. Ubarikiwe sana!

 

LATEST VIDEOS

Newsletter

Subscribe to Wapo Mission International weekly Newsletter.

Do you need JESUS as your personal savior?
If YES then Click HERE
Please rate our website

Need To Reach Us?

Email:

info@wapo.or.tz

Phone:

|+255 766 777 126 |
|+255 713 649 865 |
|+255 712 249 724 |
Do you need JESUS? Click here

Who's Online

We have 28 guests and no members online